Mvua Kuendelea Kunyesha Mikoa Hii

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo kuanzia saa tatu usiku huu wa April 3 katika maeneo mbalimbali nchini.

TMA imeyataja maeneo yatakayokumbwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua kuwa ni pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba, Mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Kigoma, Tabora na Katavi.

Kwingine ni Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Morogoro, Tanga, Dar es Salaam, Mbeya, Songwe, Rukwa, Njombe, Mikoa ya Pwani ikijumuisha Visiwa vya Mafia, Mwanza, Shinyanga, Kagera, Geita, Mara na Simiyu.

Mikoa ya Iringa, Dodoma na Singida inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, Mvua katika maeneo machache na vipindi vya Jua.

Kwa Taarifa zaidi pamoja na Viwango vya joto katika maeneo mbali mbali nchini tazama hapa chini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *