Rais Samia Afanya Uteuzi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameunda Kamati ya Kutathmini utendaji kazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ili kuiwezesha Wizara hiyo kutekeleza Malengo ya Serikali katika kukuza diplomasia ya uchumi na ushirikiano wa kimataifa.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus jana Machi 28 imeeleza kuwa, ili kutekeleza azma hiyo, Rais Samia amemteua Balozi Yahya simba, aliyekua Balozi wa Tanzania nchini Zambia kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo.

Rais Samia pia amewateua wengine wanne kuwa wajumbe wa kamati hiyo ikiwa ni pamoja na Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi Katibu wa baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mstaafu.

Wengine ni Balozi Dkt. Mwanaidi Sinare Maajar, aliyekua Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Balozi Peter Allan Kalaghe, aliyekua Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na Balozi Tuvako Nathaniel Manongi aliyekua Mwakilishu wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa New York, Marekani.

Kamati hiyo inatarajiwa kuzinduliwa tarehe 31, Machi mwaka huu saa 8:30 mchana Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *