Mvua Kubwa Kunyesha Mikoa Hii Jumanne Machi 28

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la Mvua Kubwa inayotarajiwa kunyesha siku ya  Jumanne Machi 28 katika baadhi ya maeneo nchini.

TMA imeyataja maeneo ambayo mvua hizo zinatarajiwa kunyesha kuwa ni maeneo machache ya Mikoa ya Morogoro, Mtwara, lindi na Pwani ikijumuisha Visiwa vya Mafia.

TMA imezitaja athari zinazoweza kujitokeza kuwa ni pamoja na baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja na ucheleweshwaji wa shughuli za kiuchumi na usafirishaji.

TMA imeongeza kuwa, uwezekano wa mvua hizo kutokea ni wa wastani na kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni wastani.

Aidha, TMA imefafanua kuwa, mvua zinaendelea kunyesha katika maeneo mengi yaliyosalia nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *