Mvua Kubwa Kunyesha Mikoa Hii Kesho Machi 22

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo kuanzia saa tatu usiku huu wa Machi 21 katika maeneo mbalimbali nchini.

TMA imeyataja maeneo yatakayokuwa na hali ya mawingu, mvua pamoja na ngurumo katika baadhi ya maeneo na vipindi vifupi vya jua kuwa ni Mikoa ya Mtwara na Lindi.

Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Mkoa wa Pwani ukijumuisha visiwa vya Mafia na Visiwa vya Unguja na Pemba  vinatarajiwa kuwa na hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vifupi vya jua.

kwingineko maeneo ya   Morogoro, Dodoma, Singida, Kigoma, Tabora, Katavi, Arusha, Kilimanjaro, manyara, Mwamza, Shinyanga, Kagera, Geita, Mara, Simiyu, Songwe, Rukwa, Njombe, Mbeya, Iringa na Ruvuma, kunatarajiwa kuwa na hali ya mawingukiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache pamoja na vipindi vya jua.

Katika hatua nyingine, TMA imetoa angalizo la vipindi vya Mvua Kubwa vinayotarajiwa siku ya Jumatano Machi 22 katika maeneo mengi ya Mikoa ya Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Mkoa ya Pwani ukijumuisha visiwa vya Mafia na Visiwa vya Unguja na Pemba.

TMA imezitaja athari zinazoweza kujitokeza kuwa ni pamoja na baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja na ucheleweshwaji wa shughuli za kiuchumi na usafirishaji.

Kwa taarifa zaidi na kwa viwango vya joto katika maeneo mbalimbali nchini, tazama hapa chini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *