TMA Yatoa Tahadhari Mvua Kubwa Mikoa Hii leo Machi 20 na Kesho

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la Mvua Kubwa inayotarajiwa kunyesha siku ya Jumatatu Machi 20 na Jumanne Machi21 katika baadhi ya maeneo nchini.

TMA imefafanua kuwa mvua hizo zinatarajiwa kunyesha katika maeneo mengi ya Mikoa ya Dar es Salaam, Lindi, Mtwara na Mkoa ya Pwani ukijumuisha visiwa vya Mafia.

TMA imezitaja athari zinazoweza kujitokeza kuwa ni pamoja na baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja na ucheleweshwaji wa shughuli za kiuchumi na usafirishaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *