Mvua Kunyesha Mikoa Hii Kesho Ijumaa Machi 17

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo kuanzia saa tatu usiku huu wa Machi 16 katika maeneo mbalimbali nchini.

TMA imeyataja maeneo yatakayokuwa na hali ya mawingu, mvua pamoja na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vifupi vya jua kuwa ni Mikoa ya Ruvuma, Kigoma, Katavi, Kusini mwa Mkoa wa Morogoro, Mwanza, Shinyanga, Kagera, Geita, Iringa, Rukwa, Songwe, Njombe na Mbeya.

Mikoa ya Mara, Simiyu,  Tabora na Singida inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Maeneo ya Dodoma, Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara yanatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache pamoja na vipindi vya jua.

Kwingineko Mikoa ya  Dar es Salaam, Tanga, Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, Visiwa vya Unguja na Pemba, Mkoa wa Pwani ukijumuisha Visiwa vya Mafia kunatarajiwa kuwa na hali ya maingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Mikoa ya Mtwara na Lindi inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.

Kwa taarifa zaidi na kwa viwango vya joto katika maeneo mbalimbali nchini, tazama hapa chini.

pp

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *