Mvua Kunyesha Mikoa Hii Kesho Alhamis Machi 15

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo kuanzia saa tatu usiku huu wa Machi 15 katika maeneo mbalimbali nchini.

TMA imeyataja maeneo yatakayokuwa na hali ya mawingu, mvua pamoja na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vifupi vya jua kuwa ni Mikoa ya Ruvuma, Iringa, Rukwa, Songwe, Njombe na Mbeya.

Kusini mwa Mkoa wa Morogoro, Dodoma, Singida, Kigoma, Katavi, Tabora, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Mwanza, Shinyanga, Mata Simiyu, Kagera na Geita inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Maeneo ya Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, Dar es salaam, Tanga, Visiwa vya Unguja na Pemba na mkoa wa pwani ukijumuisha visiwa vya mafia  yanatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache pamoja na vipindi vya jua.

Kwingineko Mikoa ya Mtwara, Lindi, kunatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.

Kwa taarifa zaidi na kwa viwango vya joto katika maeneo mbalimbali nchini, tazama hapa chini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *