TMA Yatoa Tahadhari Mvua za Ngurumo na Radi Mikoa Hii

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la Mvua Kubwa inayotarajiwa kunyesha siku ya Jumatano  Machi 15 katika baadhi ya maeneo nchini.

TMA imeyataja maeneo yatakayokumbwa na mvua hizo zikiambatana na mvua hizo kuwa ni maeneo machache ya Mikoa ya Mara, Simiyu, Shinyanga, Mwanza, Iringa, Mbeya, Songwe, Njombe, Rukwa, Katavi, Tabora, Kigoma, Singida, Dodoma, Ruvuma pamoja na Kusini mwa Mkoa wa Morogoro.

TMA imezitaja athari zinazoweza kujitokeza kuwa ni pamoja na baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja na ucheleweshwaji wa shughuli za kiuchumi na usafirishaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *