Manara Awamwagia Sifa Zuchu na Diamond, Afunguka Kulipa Mahari

Mnogeshaji maarufu wa masuala ya  michezo Haji Manara amewamwagia Sifa wasanii Nasibu Abdul maarufu kama Diamond Platnumz na Zuhura (Zuchu) juu mambo mbali mbali na tabia zao kwa ujumla.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram jana Machi 13 manara aliposti video ya Zuchu ikisindikizwa na ujumbe mrefu kumhusu msanii huyo.

Manara ameandika kuwa hajui kwa nini  anampenda Zuhura ila ni mtu mnyenyekevu sana na mwenye akili na kubwa anajua sana kuimba kuliko watu wanavyodhani.

Amesema, Zuchu ni miongoni wa mabinti pekee bongo wanaoandika mashairi na uimbaji wake upo juu ya upeo wa masikio ya watu na tone zake zinazidi uwezo wa watu kutambua anachoimba.

Kuhusu mahusiano ya Zuchu na Diamond  Manara amefunguka kuwa siku Diamond akitoa posa Mahari atalipa yeye.

Wallah Siku Yule Mtu mbishi akipeleka Posa tu hapa, Mahari nalipa mimi. Halaf pamoja na kumtania Kwa heshma ya mdogo wangu, lakini ana adabu mno, msikivu, mcheshi kisha Mpishi, Nyumba ya Mwanamme wa kiafrika anaiweza, Sijui huyu Shomvi anachelewesha nini !! Au Tumroge nini ?”

Imagine Sherehe za harusi ziwe Zanzibar Katika Msikiti ule mzuri wa Mabuluu, kisha kesho yake tunalisha Waunguja Mpunga pale Amani Stadium, halaf tunakuja kufanya Bonge la Party Kwa Mkapa, nyieeee nyieeee.

Kila siku Cha ubishi ananisema nisije kuthubutu kumuacha @rubynah_bnt_salum, lakini yeye ukimwambia hili lake, anaruka ruka kama ulimbo, ila Mwaka huu nnae Inasomeka sehemu ya ujumbe wa Manara.

 

Kuhusu Diamond Manara alimsifia kutokana na uhuzuriaji wake kwenye sherehe ya Hakika ya mtoto wake mdogo aitwaye Ghalib na kujumuika pamoja nao.

 

Uzuri wa Nassib anajua amsha amsha sana, Kafika home, direct na team yake wameenda kuserebuka, halaf anatokea mtu kafluk nyimbo moja au mbili, ananiletea pozi eti

Imagine jamaa toka Mchana nipo nae home, ameenda kisha amerudi tena Usiku, kesho ukiona nampa Maugali yake, unasema ooooh unabagua.

Mtu ambae keshawahi kukataa Show ya Mamilioni Nairobi ili tu awahi birthday party yangu, Namuachaje Kwa mfano? Mtu aliyehama hadi team kunifata ndugu yake, nakosaje kumweka mbele.

Guys anaekufata ndio nduguyo, na wewe mfate, muunge mkono bila haya, mshike Coz wengi wetu hatupendani, tunachekeana usoni tu, na kusemana semana hovyo, kisha kuoneana choyo kibwege.

Once again, Shukran sana Ndugu zangu wa @wcb_wasafi , hamjawahi kuniacha kwa lolote lile na mimi siwezi kuwaacha, always events zangu mnanipa full coverage, mmeshirikiana vema na Media yetu ndogo ya @manaratv__ kutupeleka Mjini.

Nb:: Sikieni nyie, Bongo ina Wasanii wengi wazuri ila Msanii mkubwa ni mmoja tu, Case Closed.” Inasomeka sehemu ya Ujumbe wa Manara.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *