Diamond Afunguka Kuweka Picha ya Marehemu Costa Titch

Kufuatia Kifo cha Msanii maarufu toka South ambaye alifariki dunia ghafla baada ya kuanguka jukwaani wakati akifanya Shoo usiku wa Jumamosi, Diamond Platnumz ametoa ya moyoni kuhusu msiba huo.

Diamond alibadili Picha yake ya utambulisho ya Instagram (DP) na kuzua gumzo mtandaoni huku mashabiki wengi wakitamani kujua kwa nini alifanya hivyo.

Akizungumza katika kipindi cha the Switch cha Wasafi FM jana  Jumatatu Machi 13 Diamond amesema kuna misiba mingi imetokea lakini msiba wa Costa Titch umemgusa sana sababu marehemu alikua kama familia kwake na alikua mnyenyekevu sana.

“Alikua Mwanangu sana halafu aliniheshimu na kunikubali, vijana wengi wanaotoa nyimbo wakafanya vizuri kwa kiwango cha Costa wengi wanakua hawana discipline,” alisema Diamond.

Alisema, yeye na Marehemu walikua wanaheshimiana sana, hawajawahi kuvunjiana heshima na wameishi kifamilia na kupeana sapoti kwenye kazi mbali mbali za kisanii.

Diamond aliongeza kuwa, Marehemu alikua mtu real sana na wamekua wakisapotiana katika mambo mbali mbali yeye akienda South Africa na Costa akija TZ.

“Mara ya mwisho nimeongea nae kifo cha AKA juzi, yaani naambiwa amekufa nimestaajabu, sababu alikua mdogo sana ana miaka 28, nimemzidi Zaidi ya miaka mitano kibinaadamu nilifikiria ingetangulia mimi angefuata yeye maana kiumri mimi nimetangulia, mara naambiwa kadondoka,” Aliongea Diamond.

Titch na Diamond wamewahi kufanya wimbo uitwao Superstar, mbali naye, alifanya kazi na wasanii wengine akiwemo Mbossona Rayvanny.#

 Zaidi, Msikilize Diamond hapa Chini

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *