Mvua Kunyesha Mikoa Hii Kesho Jumamosi machi 11

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo kuanzia saa tatu usiku huu wa Machi 10 katika maeneo mbalimbali nchini.

TMA imeyataja maeneo yatakayokuwa na hali ya mawingu, mvua pamoja na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vifupi vya jua kuwa ni Mikoa ya Ruvuma, Kusini mwa Mkoa wa Morogoro, Kigoma, Katavi, Tabora, Iringa, Rukwa, Songwe, Njombe, Mbeya, Mwanza, Shinyanga, Kagera, Geita, Mara na Simiyu.

Mikoa ya Dodoma na Singida inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Maeneo ya Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, Arusha, Manyara na Kilimanjaro inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache pamoja na vipindi vya jua huku Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Mtwara, Lindi, Visiwa vya Unguja na Pemba, Mikoa ya na Mkoa wa pwani ukijumuisha Visiwa vya Mafia ikitarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.

Kwa taarifa zaidi na kwa viwango vya joto katika maeneo mbalimbali nchini tazama hapa chini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *