Wakenya: Samia Suluhu Katupiga Kijembe

“Ndugu zangu nataka niwaambie Tanzania iko vizuri kiuchumi ukilinganisha na majirani zake katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki sisi ni bora kuliko nchi nyingine mtu asikudanganye sasa hivi kila nchi inalalamika kukosa dola ingawa tunazo za kutosha kwa miezi minne,” 

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu, amewahakikishia wananchi wake kuwa nchi iko katika hali nzuri kiuchumi, tofauti na baadhi ya majirani ambao hakuwataja. Rais Samia Suluhu asema Tanzania ina dola nyingi kuliko majirani zake.

Akizungumza siku ya janaJumatano, Siku ya Wanawake Duniani, Samia alisema kuwa Tanzania imeimarika kiuchumi kwani ia pesa ziada kwenye hazina yake kuliko nchi nyingine  za Afrika Mashariki.

Watu nmbalimbali walitoa maoni yao juu ya alichoongea kiongozi huyo katika mitandao ya kijamii na wengi wao walionekana kufanya utani kwa kumanisha kuwa Rais alikusuidia kuisema nchi jirani ya Kenya.

Na haya hapa ni baadhi ya maoni;

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *