Mvua Kunyesha Zaidi ya Mikoa 20 Kesho Ijumaa Machi 10

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo kuanzia saa tatu usiku huu wa Machi Tisa katika maeneo mbalimbali nchini.

TMA imeyataja maeneo yatakayokuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua pamoja na ngurumo katika maeneo macheche na vipindi vya jua kuwa ni Mikoa ya Ruvuma, Kusini mwa Mkoa wa Morogoro, Kigoma, Katavi, Tabora, Singida, Iringa, Rukwa, Songwe, Njombe, Mbeya, Mwanza, Shinyanga, Mara na Simiyu.

Mikoa ya Kigoma, Dodoma, Kilimanjaro, Arusha na Manyara inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara, Lindi, Tanga, Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, Tanga, Mkoa wa Pwani ukijumuisha Visiwa vya Mafia pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.

Kwa taarifa zaidi na kwa viwango vya joto katika maeneo mbalimbali nchini tazama hapa chini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *