TMA Yatoa Utabiri Hali ya Hewa Nchini

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo kuanzia saa tatu usiku huu wa Machi saba katika maeneo mbalimbali nchini.

TMA imeyataja maeneo yatakayokuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua pamoja na ngurumo katika maeneo macheche na vipindi vya jua kuwa ni Mikoa ya Ruvuma, Rukwa, songwe, Iringa, Njombe, Mbeya.

Mikoa ya Kigoma, Katavi, Kagera na Geita inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Tanga, Tabora, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Lindi, Mtwara, Singida, Dodoma, Mwanza, Mara, Simiyu, Shinyanga na Mkoa wa Pwani ukijumuisha Visiwa vya Mafia inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.

Kwa taarifa zaidi na kwa viwango vya joto katika maeneo mbalimbali nchini tazama hapa chini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *