Mvua kunyesha Mikoa Hii Usiku Huu na Kesho Jumamosi Machi 4

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo kuanzia saa tatu usiku huu wa Machi tatu katika maeneo mbalimbali nchini.

TMA imeyataja maeneo yatakayokuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua pamoja na ngurumo katika maeneo macheche na vipindi vya jua kuwa ni Mikoa ya Dodoma, Singida, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Kusini mwa Mkoa wa Morogoro, Tabora, Kigoma, Katavi, Rukwa, songwe, Iringa, Njombe, Mbeya, Mwanza, Kagera, Geita, Shinyanga, Mara na Simiyu.

Mikoa ya Arusha, Manyara na Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Kilimanjaro, Visiwa vya Unguja na Pemba, na Mkoa wa Pwani ukijumuisha visiwa vya Mafia inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.

Kwa taarifa zaidi na kwa viwango vya juu vya joto tazama hapa chini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *