Tahadhari Mvua, Hali Mbaya ya Hewa Maeneo Haya Kesho Ijumaa Machi 3

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la hali mbaya ya hewa inayotarajiwa siku ya Ijumaa Februari tatu katika baadhi ya maeneo nchini.

TMA imetoa angalizo la mvua kubwa kwa siku ya Ijumaa Machi tatu katika maeneo ya Mikoa ya Mara, Simiyu, Shinyanga, Mwanza, Dodoma na Singida.

Angalizo la upepo mkali unaofikia Kilomita 40 kwa saa limetolewa kwenye baadhi ya maeneo ya Pwani ya Kusini mwa Bahari ya Hindi inayojumuisha mikoa ya Lindi na Mtwara.

TMA imezitaja athari zinazoweza kujitokeza kuwa ni pamoja na baadhi ya makazi kuzungukwa na maji pamoja na ucheleweshwaji wa shughuli za kiuchumi na usafirishaji.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *