Chadema Wataja Chanzo Kagera Kuwa Maskini

Mwenyekiti wa Chadema Kagera, Mechard Rwizile amesema mji wa Kagera ni umedumaa licha ya kuwa mji ambao ungepaswa kukua haraka.

Akizungumza katika mkutano wa chama hicho Kagera leo Februari 27 Rwizile ameeleza  historia fupi na kusema kuwa, mwaka 1967 zilitaifishwa mali za watu nchini.

Aliongeza kuwa, mnamo mwaka 1972, vilifungwa vyama vya ushirika ambavyo vilichangia kukuza uchumi, kusomesha watu na kuleta maendeleo ya msingi.

Aidha, Rwizile alisema, mwaka 1961 wakati wa kupata Uhuru, Mkoa wa kagera ulikua kati ya mikoa bora nchini.

“Tulikua na watu wataalamu waliosoma, wako New york, wako London wanaleta mapato katika mkoa huu, ulikua umeendelea, sasa hivi ni mkoa wa mwisho katika maendeleo, ” alisema Rwizile.

Amesema leo hii, mji umeharibika, umebaki magofu na maendeleo ni kidogo kwa sababu ya katiba mbovu inayoamua nini lifanyike.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *