Mwendokasi Lavamia Nyumba Likikwepa Gari

Basi la Mwendokasi lililokuwa likifanya safari zake kutoka Kivukoni kuelekea Kimara Mwisho limepata ajali asubuhi hii baada ya kuacha njia ya kugonga moja ya majengo yaliyopo pembezoni, karibu na makutano ya barabara ya Jamhuri na Morogoro.

Taarifa kutoka kwa mashuhuda zinaeleza kuwa ajali hiyo imesababishwa na gari jingine kujaribu kuvuka bila tahadhari na hivyo kumlazimu dereva wa mwendokasi kumkwepa na kugonga jengo lililokuwa eneo hilo.

Aidha, majeruhi kadhaa ambao wengi wao ni abiria wa basi hilo wamekimbizwa hospitali kwa ajili ya kupata matibabu.

Chanzo: Nipashedigital

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *