Halima Mdee Ajibu Shutuma Kuinyatia ACT Wazalendo

Mbunge Viti Maalum kutoka Kambi ya Upinzani, Halima Mdee amejibu shutuma zilizoandikwa na gazeti la Raia mwema juu yake na wenzake kuwa Wanakinyatia chama cha ACT Wazalendo.

Mdee na Wenzake wamekua na mgogoro na chama chao cha CHADEMA kufuatia wabunge hao kutumikia nafasi za ubunge viti maalum kinyume na matakwa ya chama hicho.

Februari 19, Kupitia Ukurasa wake wa Twitter Mdee aliwapongeza Zitto Kabwe na timu nzima ya ACT Wazalendo kutokana na mkutano mkubwa wa kisiasa walioufanya siku hiyo Mbagala Jijini Dar es Salaam.

Leo Februari 22 Gazeti la Raia Mwema limeandika kuwa Mdee na wenzake wanatia ACT. Mdee alijibu shutuma hizo kwa kuandika haya katika ukurasa wake wa Twitter

“Kwa hiyo TUKITAMBUA jambo jema linalofanywa na wenzetu, ni ‘KUINYATIA’?..UZURI hata MWANDISHI (MMILIKI wa GAZETI) anajua CHAMA changu..ni SUALA la MUDA tu.Kama ingekuwa kutambua ZURI la wengine ni ‘KUNYATIA’..basi tuna ‘WANYATIAJI’ wengi sana NCHI HII.” Aliandika Mdee

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *