RC Mbeya: Kuna Gereza Ndani Lina Madini, Tutalihamisha

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera ameeleza jinsi mkoa huo ulivyobarikiwa madini mbali mbali hivyo kusaidia katika kukuza uchumi.

Akizungumza katika kipindi cha Clouds360 leo Februari 16 Homera amesema Mbeya ni mkoa wa pili kwa dhahabu nchini ambapo kumegawanyika kuna Chunya na Mbeya.

Amefafanua kuwa, Chunya peke ake inazalisha dhahabu kilo 334 – 350 kwa mwezi na inakimbilia kwenye Tani.

RC Homera ameyataja madini mengine yanayopatikana Mbeya kuwa ni Neobum na kwamba kuna Gereza lina madini hayo hivyo itabidi lihamishwe kutokana na umuhimu wa madini hayo.

“Ndani ya gereza letu mojawapo kuna madini ya Neobium sasa tutahamisha gereza. Madini hayo yanatumika kutengeneza injini za ndege, vipuri vya ndege, bati la ndege, madaraja makubwa unayoyaona Tanzania kama Tanzanite, daraja la Magufuli yote yanatengenezwa na madini kutokea Mbeya”

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *