Breaking: Profesa Lipumba Apata Ajali, Gari Lapinduka

Mwenyekiti wa Chama Cha CUF Tanzania, Ibrahim Lipumba amepata ajali mbaya ya gari akiwa mkoani Lindi Katika harakati za kisiasa.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo leo Februari 16 Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano ya Umma wa CUF, Injinia Mohammed Ngulangwa amesema wa  baada ya kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa hadhara uliofanyika wikiendi iliyopita, Profesa lipumba alialikwa katika harakati za Ujenzi wa Chama katika mkoa wa Lindi, hususani Kilwa.

Amesema, jana Profesa alikua na mkutano katika eneo la Njinjo na alipokua akitokea Njinjo kuelekea Kivinje akiwa njiani eneo la Nangurukuru gari yake ilipata ajali.

“Gari Ilipinduka, tunachoshukuru pamoja na kwamba gari iliharibika vibaya, lakini waliokuwepo ndani, akiwemo na profesa lipumba wamesalimika”

Injinia Ngulangwa amesema, kati ya hao, Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu na sheria Mhe Salvatory alipata majeraha madogo.

Amesema, watu wote wanaendelea vizuri kwa sasa ingawa ni kweli ajali hiyo imeharibu kabisa gari ya Profesa Lipumba.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *