Mbosso Apata Ajali Huko Marekani

Msanii anayefanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Fleva Mbosso Khan amepata ajali usiku wa kuamkia leo Februari 15, akiwa Marekani kwenye safari ya kimuziki.

Kupitia Mtandao wake wa kijamii wa Instagram (Instastory) Mboso alipakia video akionyesha madhara ya ajali hiyo yalivyokua.

Mbosso alionyesha jinsi gari nyingine ilivyogonga upande aliokua amekaa yeye ambapo ni siti ya mbele ya abiria.

Hata hivyo, mbosso hakusita kuwajuza mashabiki wake hali yake kiafya kufuatia tukio hilo kwamba yuko salama na amepata maumivu kiasi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *