Shabiki Yanga Yamkuta, Afunguka Kusafisha Ofisi Simba

Picha haihusiani na tukio

Ofisa Habari wa Tawi la Yanga Miomboni Mkoani Iringa, John Njala, amelazimika kufanya usafi katika ofisi ya Simba tawi la Kihesa kama mojawapo ya ahadi aliyoweka iwapo Yanga watafungwa na US Monastir katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Akiongea  na Joseph Mpangala wa Azam TV jana Februari 13 mara baada ya kutimiza ahadi yake, John Njala amesema, amelazimika kutimiza ahadi hiyo.

“Hii ahadi tuliekeana na bwana Obed toka siku ya juzi, nilimuahidi kwamba nikifungwa ntakuja kufanya usafi eneo lake la kazi na kweli nimeenda nimepasuka Tunisia goli mbili bila, kwa hiyo nahitaji niitimize ahadi ambayo niliweka sababu mpira si uadui, ni urafiki na undugu ,” alisema Njala.

Naye Shabiki nakiongozi wa tawi la Simba Kihesa Obedi Lupenza amesema, ahadi zote wanazowekeana ni lazima zitimizwe.

“Wana midomo sana, kwa hiyo hata Viongozi na Wachezaji wao wajue kuna mashabiki wanaumia kwa sababu yao,  yule kijana (Njala) anaumia sana kachubuka mikono lakini lazima atimize ahadi,” alisema Lupenza

Naye Njala baada ya adhabu hiyo alitoa ahadi nyingine kwa Lupenza kwamba wasipotoboa robo fainali ampe kazi yoyote anayoiona ngumu hata ya kushusha injini.

Zaidi watazame watani hao wajadi wakitambiana kwenye video hapa chini

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Azam Sports (@azamtvsports)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *