Keysha Afunguka Ishu ya Diamond

Staa wa Muziki wa Bongo, Keysha ambaye hivi Karibuni amezindua album yake ya Mwangaza, amefunguka kuhusu uwepo wa Diamond kwenye Album hiyo.

Akijibu swali la East African Radio leo Februari 13 kuhusu kukosekana kwa Diamond lakini kuwepo kwa Ally kiba kwenye Album yake Keysha amesema yeye ni msanii wa kwanza wa kike kufanya kazi yake mwenyewe na diamond huko nyuma.

“Diamond ni Msanii mkubwa, ana nafasi yake hamna mtu anayeweza aka ignore hiyo, lakini nashukuru pia kwenye ile event mafanikio ni makubwa sababu kulikua na wasanii wengine pia ambao pia ni wakubwa,”alsema Keysha.

Keysha aliongeza kuwa, Diamond kuwepo au kutokuwepo kwenye album yake haijaleta tofauti kubwa kwani alikuepo Alikiba na imezungumziwa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *