Jinsi ya Kulinda Figo Zako

Je wafahamu figo ni kiungo muhimu sana katika mwili?o Huondoa takamwiliu, huleta msawaziko wa maji na madini mwilini, huboreshs afya ya ya mifupa, utengezaji damu nk.

Norman Jonas, Daktari na Mtaalamu wa masuala ya Afya ya jamii anatuelezea baadhi ya hatua unaoweza kufanya ili kulinda afya ya figo yako.

1. Dhibiti Magonjwa ya Kudumu Kama Kisukari na Shinikizo la Damu

Maradhi ya kudumu kama kisukari na shinikizo la damu huweza kuharibu figo zako kadri muda unavyokwenda, hivyo ni muhimu kuhakikisha yamedhibitiwa.

2. Zingatia Unywaji Maji

Kiwango cha maji mwilini huweza kuathiri utendaji kazi wa figo; muhimu kuzingatia unywaji maji hasa kama huna ugonjwa wa moyo au figo.

3. Angalia Matumizi Yako ya Chumvi

Chumvi hupandisha shinikizo la damu ambalo huweza kuathiri figo. Ni muhimu kuzingatia ulaji chumvi kidogo, unashauriwa kutozidi kijiko kidogo kwa siku.

4. Zingatia Mazoezi

Mazoezi hutoa kinga dhidi ya maradhi kama kisukari na shinikizo la damu ambayo huweza kuathiri figo yako.

5. Zingatia Mlo Bora

Mlo bora hujumuisha matunda, mboga za majani, nafaka zisizokobolewa na nyama nyeupe kama samaki.

6. Epuka Sigara na Dhibiti Pombe Kupita Kiasi

7. Pima Afya Walau Kila Mwaka

Upimaji afya kwa ujumla ukijumuisha na kupima protini kwenye mkojo na ufanyaji kazi wa figo husaidia kugundua maradhi ya figo mapema na kuwahi tiba ya kuzuia uharibifu kuendelea.

8. Usitumie Dawa Hovyo

Tumia dawa kama ulivyoelekezwa na mtoa huduma za afya vilevile

MUHIMU: Endelea kujielimisha kuhusu afya, unapopata mabadiliko ya kiafya nenda kituo cha kutolea huduma upate uchunguzi na tiba sahihi, afya yako mtaji wako.

Chanzo: Dr. Norman Jonas Tweets

https://mobile.twitter.com/NormanJonasMD

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *