Ufaransa Yawabana Waangalia Filamu za Ngono

Waziri wa Dijitali wa Ufaransa Jean-Noel Barrot alisema kuwa idara yake itaanzisha kile anachodai kuwa ni utaratibu wa kwanza duniani wa uidhinishaji wa umri wa kidijitali ambao unawazuia kwa usalama watoto wachanga kupata tovuti za ponografia.

Wanaotembelea tovuti za maudhui ya watu wazima kwanza watapakua programu (APP) ya serikali ili kuthibitisha kuwa wana umri wa angalau miaka 18.

Kulingana na kura ya maoni ya tovuti ya serikali ya 2018, karibu mtoto mmoja kati ya watatu walio na umri wa chini ya miaka 12 nchini Ufaransa ameonyeshwa ponografia mtandaoni, na hivyo kuongezeka hadi 62% ya watoto kufikia umri wa miaka 15.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *