Kumbe Zuchu ni Mama Kijacho!

Kutokana na nyepesi nyepesi za mjini Instagram, msanii Zuchu anasemekana kuwa na ujauzito wa mpenzi wake Diamond Platnumz.

Wakali wa kuunganisha matukio wamelithibitisha hilo kutokana na msanii Diamond jioni ya leo Februari 7 kupitia Insta stori yake kuposti ya kwamba ni wakato wa yeye kuongeza mtoto.

Muda kidogo baada ya ujumbe huo wa Diamond, Zuchu alipost kionjo cha wimbo wake mpya atakaoutoa Februari 10 ambapo kaka wa Diamond, Romy Jones aliandika komenti iliyosomeka ‘mama kijacho’.

Kufuatia hayo Mashabiki waliunganisha matukio wapo walio koment inawezekana kweli ni zuchu ni mama Kijacho huku wengine wakiwa hawaamini wakidhani kuwa ni kiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *