Kionjo Ngoma Mpya ya Zuchu Hiki Hapa, Diamond Atia Neno

Nyie WCB hawapumziki kabisa, ni ngoma juu ya ngoma. Hayo yamethibitishwa na mwanadada anayefanya vizuri katika anga za mziki Afrika Mashariki kwa kuwapa mashabiki kionjo cha wimbo wake mpya.

Kupitia ukurasa wa Instagram leo Februari 7 ameposti kipande cha wimbo wake huo mpya na kueleza kuwa utatoka rasmi Februari 10.

Bosi na mpenzi wa msanii huyo Diamond Platnumz hakuwa nyuma na kutumia ukurasa huo kuandika kuwa hiyo ni nyimbo yake ishara ya kuwa anaupenda wimbo huo.

Mashabiki nao hawakua nyuma kuonyesha kuguswa kwao na wimbo huo. Zaidi kionjo cha wimbo huo na pitia koment hapa chini.

 

 

View this post on Instagram

 

A post shared by ZUCHU (@officialzuchu)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *