Haji Manara Awaomba Mashabiki Kumuombea Binti Yake

Kufuatia Janga la tetemeko la ardhi linaloikumba nchi ya Uturuki, Haji Manara amewaomba mashabiki zake kumuombea binti yake na wote waliokuwa huko wanaokabiliwa na janga hilo.

Haji ambaye binti yake yupo Uturuki kimasomo, ameandika ujumbe katika ukurasa leo Februari 6 akielezea anavyojiskia.

“Poleni sana Wananchi wa Uturuki Kwa janga hili kubwa linaloumiza ubongo wangu.

Nakulaje au Nalala vipi ikiwa mwanangu yupo huko Kwa sasa?

Nimezungumza nae kaniambia leo Media ya huko imesema, Majiji ya Istambul na Ankara yanatarajiwa kupata Matetemeko mengine ya Ardhi, hivyo wameamua kukaa nje ya majengo kama walivyoshauriwa kitaalamu.

Kila nikifikiria na Baridi ya huko hivi sasa naogopa mno na imebakia Dua tu na nimemsisitiza sana kuendelea kumuomba Mola awaepushe na huu mtihani.

In fact nimekuwa Shocked na labda Ofisi za Balozi zetu na zao zitatushauri tufanye nini ? May be kuangalia uwezekano wa yeye Kurudi Tanzania katika kipindi hiki.

Naomba dua zenu kwa wote waliokuwa huko na Mungu awasallimu salama Insha’Allah” Unasomeka ujumbe wa Manara.

Vyombo vya habari vimeripoti takriban watu 76 wamepoteza maisha katika tetemeko la Ardhi nchini Uturuki na wengine kujeruhiwa na kusababisha uharibifu wa maje go kusini mwa nchi hiyo.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Haji Sunday Manara (@hajismanara)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *