Ruti Mpya za Kigamboni, Wenye Daladala Wakaribishwa

Mamlaka ya Udhibitu Usafiri Ardhini (LATRA) inawakaribisha wasafirishaji kuomba leseni kwenye njia mpya za daladala Dar es Salaam ili kufikisha huduma kwa wananchi.

Wito huo uliotolewa leo Februari 3 na Latra unahusu mabasi yanayokidhi vigezo na kwa gari mpya ambazo hazijawahi kusajiliwa katika mfumo wa utoaji leseni wa PRIMS dereva husika atapaswa kuthibitishwa LATRA.

Miongoni mwa ruti hizo ni toka Kinyerezi kwenda Simu 2000 kupitia barabara Mandela, Kibada stendi kwenda Mbezi Luis kupitia barabara ya Mandela, Darajani na Morogoro

Ruti zingine ni toka Kibada Stendi kuenda Simu 2000, Temeke Mwisho, Tabata Segerea, Tegeta Nyuki, Kigogo Sokoni na Pugh Stesheni kwenda Kawe.

Kwa ruti zote hizo ujazo wa abiria ni kuanzia 25, kwa ufafanuzi zaidi wa ruti hizo na barabara zinapopita tazama hapa chini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *