Zitto amtaka Biswalo, Jaji Mkuu Kujiuzulu

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amewataka Jaji Mkuu na Jaji Biswalo wajiuzulu ili kupisha uchunguzi na kulinda hadhi ya mahakama.

Hayo yamesemwa leo Februari 2, katika taarifa ya Ofisi ya Kiongozi wa Chama iliyotolewa na Zitto katika ukurasa wake wa twitter.

Zitto amesema kuwa taarifa hiyo wameitoa kufuatia hatua ya Rais Samia juzi Januari 31 kuapisha Kamati ya Kupitia Haki Jamii Nchini na pia kutoa taarifa kuhusu sehemu kubwa ya mabilioni ya fedha yaliyokusanywa kwa mtindo wa Plea Bargain na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP) kutojulikana yalipo.

“Kwa maelezo hayo ya Rais, aliyekua Msimamizi Mkuu wa Mhimili wa Haki nchini ambaye bado ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Ndugu Jaji Ibrahim Juma na aliyekua DPP wa wakati wa uvunjifu huo wa haki Jaji Biswalo Mganga hawana sifa ya kuendelea kutumikia nyadhifa za kisheria walizonazo sasa.” Ilisema taarifa hiyo ya Zitto

Zitto alifafanua sababu ya ACT kuwataka wajiuzulu kuwa ni kupisha uchunguzi wa kina wa jambo hilo na pia kusitiri mhimili wa Mahakama ambao ulinajisiwa mbele ya macho yao.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *