Rushayna Afunguka kurudiana na Manara

Baada ya maneno mengi kusemekana mitandaoni kuhusu kuachana kwao, Rushayna amefunguka mengi kuhusiana na kuachana kwake na Manara na mahusiano yao kwa sasa.

Leo Februari mosi wakati akitambulishwa kuwa balozi wa Emish akijibu maswali ya Waandishi amesema mpaka sasa Manara amempa talaka moja lakini hayuko tayari kurejea na wala hahitaji ndoa yoyote.

Alipohojiwa kuhusu suala la kupitia manyanyaso alisema ni kawaida tu na suala la yeye kujutia kuolewa na Manara lipo 50/50

“Kama unaona hupati amani sehemu using’ang’anie. Maisha unaweza kuayaanza hata ukiwa peke yako na unaweza ukafika unapopataka. Ni rahisi sana ukimuamini Mungu na kumtanguliza Mungu mbele” Alisema Rushyna

Aidha Rushayna amesema kuwa kwa sasa hawezi kuweka wazi kama yuko kwenye mahusiano au la.

Mbali na hilo pia pia amekanusha kuhusu uvumi unaoenea kwamba yeye alifuata pesa kwa Haji na kufafanua kuwa pesa alizonazo Haji ni za kawaida hivyo hajafuata pesa.

Kuhusu suala la yeye kukaa eda baada ya talaka Rushayna anasema halikutokea sababu kwenye kuachana kwao hawakufuata sheria.

Kuhusu mahusiano yake na Harmonize, amesema kwamba wao ni marafiki tu na kuhusu Diamond amesema hana ukaribu nae wowote.

Zaidi tazama video hapa chini

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *