Jezi ya Yanga Yapondwa Vibaya- Wameiga!

Siku ya jana bwana imeisha hivi..wanajagwani hao wamejikusanya zao na kuita wahandishi wa habari tayari kutambulisha jezi mpya ambazo watazitumia katika mashindano ya Kombe la Shirikisho hatua ya Makundi mwaka huu.

Jezi mpya hizo zimetambulishwa pamoja na mdhamini mpya kampuni ya Haier ya nchini China na deal hilo linalokaribiwa kufikia shilingi bilioni 1.5 za kitanzania.

Jezi hizo zimebuniwa na Sheria Ngowi  mwanamitindo maarufu nchini Tanzania.

Kama ilivyo ada watanzania bana hawajua kuvunga hata kidogo wameenda kufukunyua bana na kukuta ni copy and paste ya uzi maalumu wa Getafe CF wa mwaka 2021 kwa kusherehekea miaka 75 ya kuanzishwa kwake.

Privaldinho ambae ni Menejea wa Digitali wa Yanga alianza kujigamba hivi na kuandika ” Tunatoa elimu ya ubunifu. Narudia tunatoa elimu.”

Basi bwana! Si aliona kamaliza! Wabongo hao wakaanza mshushia makombora kama kawaida yao. Na hivi ndivyo walikua na haya ya kusema;

Vipi wewe unazionaje? Zinafanana? Tuandikie maoni yako turuke nayo pia kwenye taarifa zetu zinazokuja.

Kumekuwepo na maswali kwanini Yanga wameingia mkataba na kampuni hiyo  na vipi mustakabali wa Sporpesa? Kwa mujibu wa taarifa Daily Active inazo ni kuwa Yanga hawawezi kutumia jezi kwenye mashindano hayo wakiwa na logo ya Sportpesa kwakua mfadhili mkuu wa mashindano hayo ni kampuni ya kubeti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *