Rais wa Ufaransa Muongo: Erdogan

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron “si mkweli”, akisisitiza kuwa nchi yake inaamini “siasa za kimataifa zinapaswa kujengwa kwa uaminifu”.

Erdogan amezungumza maneno hayo alipokua akiwahutubia  vijana kwenye mkutano jimboni Bilecik nchini humo.

“Pale ambapo hakuna uaminifu, hakuna utu,” Erdogan alisema, na kuongeza, “Bila shaka, kuna viongozi wengi wa aina hiyo duniani.”

Erdogan alisema ni bahati mbaya kwamba “katika mahusiano na Ugiriki katika bahari ya Mediterania, wanaipuuza nchi yake kuingia katika uhusiano tofauti nao.”

Aliongeza Ufaransa inapoteza kwa kasi sifa yake barani Afrika, ikiwa ni pamoja na Mali na Burkina Faso, na katika jumuiya pana ya kimataifa.

“(Macron) amepoteza uaminifu wake bungeni … Ufaransa inapoteza uaminifu kila mara,” Erdogan alisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *