Manzoki Ashambuliwa Hatari

“Walijua nitavaa nguo za kinyoka nyoka”

Ni moja ya kauli aliyoitoa Caeszar Manzoki alipopewa nafasi ya kuongea kwenye mkutano mkuu wa Club ya Simba weekend hii. Kauli hii imepokelewa kwa uchungu mkubwa na wanajagwani mtandaoni.

Manzoki alikua akimaanisha kuwa asingeweza kuchezea timu ya Yanga kwakua mapenzi yake yake Simba.

 

“Kwa lugha za kejeli alizotoa huyu mwamba ingekuwa ni mchezaji wa Yanga ameongea wapambe wangetoka na mapanga muda huu”

Alianza kulalamika Meneja wa Digitali wa timu ya Yanga, Privadinho kupitia ukurusa wake rasmi wa Twitter. Kama hiyo haitoshi naye mtumiaji wa mtandao huo aitwae “Jkutoe”

“Ni kweli yaan Kuna tatizo Kwa waandishi wetu wa habari za michezo hakuna hata mmoja aliyepaza sauti Kwa huyu paka kutoa Lugha za kashfa Kwa yanga ila Yanga ndiyo klabu inayowaongezea followers kwenye mitandao ya kijamii”

Kama hiyo haitoshi nao mashabiki wa Simba wakajitokeza kufanya utani wao kama kawaida.

Manzoki Nyota huyo aliyekuwa akihusishwa na Simba kwa muda mrefu, alijiunga na klabu ya Dalian Pro ya nchini China akitokea kwa mabingwa wa Uganda, Vipers SC iliyokuwa inanolewa na Mbrazili Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ambaye kwa sasa yupo Simba.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *