Diamond Atoa Tamko ‘Yatapita’

Msanii Diamond Platnumz ambaye kwa sasa anatamba na kibao kipya cha ‘yatapita’ ametoa tamko kuhusu wimbo wake huo na kuibua shangwe kwa baadhi ya mashabiki.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram Diamond ameandika kuwa atachagua watu wawili atakaofanya nao remix ya wimbo wa yatapita kupitia mchakato aliouainisha.

“Najua kuna wengi wanavipaji mtaani ila bado hawajapata nafasi ya vipaji vyao kuonekana ama kusikika, na pia mada hii ya yatapita inagusa sehemu kubwa ya maisha yetu ambayo mengine sijayazungumza”

Dimaond aliongeza kuwa, ameweka beat (mdundo) wa nyimbo ya yatapita youtube ili wenye vipaji vya kurap,  kuimba au ushairi wawasilishe mawazo yao.

“Si lazima kurekodi studio kama hauna uwezo wa kifedha, unaweza kuplay beat tu na kuimba juu yake kisha jirekodi, posti na hashtag ya #yatapita nami nitakuona” aliandika Diamond

Mchakato alioueleza ndio utakaotumika na msanii huyo kuwapata watu wawili atakaoshirikiana nao kwenye remix ya yatapita.

Baada ya kuposti hayo mashabiki hawakua nyuma na wapo waliomsifia Mondi kwa hatua hiyo nakutoa yao ya moyoni.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *