Nisamehe – Kabi wa Jesus Baada ya Kumzaa Mtoto na Binamu

Wanablogu wa YouTube, Peter Kabi, maarufu kama Kabi WaJesus, na Milly Wambui, ambaye ni Milly WaJesus wa Familia ya Wajesus kwa muda mrefu sasa wamekuwa kielelezo bora wa ndoa kwenye mtandao wa kijamii.

Hatimaye, Kabi wa Jesus amethibitisha kwamba alizaa mtoto na binamu yake Shiko mnamo 2013 kabla ya kuokoka.

Miezi mitatu iliyopita, mwanablogu huyo alinikwa hadharani kwa madai ya kupuuza mtoto wake.

Baada ya habari hiyo kusambaa, Kabi, pamoja na mkewe Milly, walionyesha kutofurahishwa na jinsi wanamtandao walivyokuwa wepesi sana kukubali kuwa mtoto kwenye picha ni mpwa wake.

“Mwanadada unayemuona kwenye picha hii ni binamu yangu, na mtoto tuliyepiga naye picha hii anaitwa Abby na yeye ni mpwa wangu. Mtu anawezaje kusema wewe ni baba wa mtoto wa binamu yako?” Aliuliza.

Lakini Alhamisi, Kabi alithibitisha kuwa yeye ndiye baba mzazi wa msichana huyo wa miaka saba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *