Mwandishi Ken Walibora Aaga Dunia

Mwandishi Mkongwe wa Kiswahili na mwanahabari wa zamani wa NTV Ken Walibora aliaga dunia Ijumaa, Aprili 10, baada ya kuhusika katika ajali mbaya ya barabarani katika barabara ya Landhies, Nairobi

NTV ilikuwa ya kwanza kuripoti Jumatano, Aprili 15,kwamba mwili wa Walibora ulipatikana kwenye nyumba ya kuhifadhia maiti ya Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta baada ya kugongwa na gari.

Mwandishi huyo ana hadhi na sifa nyingi. Kati ya kazi zake maarufu ni Ndoto ya Amerika na Siku Njema. Kitabu hiki kilikuwa kitabu cha sekondari kati ya 1997 na 2003. Kidagaa Kimemwozea, kitabu kingine mashuhuri pia kilitumiwa kama kitabu cha masomo kwenye shule ya upili mnamo 2013.

Taarifa zaidi kufuatia…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *