Waziri wa Afya Mutahi Kagwe siku ya Jumatano Machi 18 alitangaza visa vingine tatu vya Corona nchini.
Tangazo hili linafikisha visa 7 sasa kwa visa vya corona ambavyo vimepatikana Kenya.
Alisisitiza kuwa watatu hao waliingia humu nchini mmoja wao akiwa raia wa Burundi aliyetoka Dubai siku ya Jumanne.

Wawili kati ya hao watatu waliwasili tarehe nne Machi walipotua kwenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta kutoka Dubai.
Kagwe alisema kuwa juhudi za kuwatafuta watu ambao wanaweza kuwa walitangamana nao zimeimarishwa.