MCA Mwingine Afariki, Siku Mbili Baada ya Kifo Cha MCA Omondi

Aliyeteuliwa MCA kutoka Meru, Petronilla Gainchi, ameaga dunia.

Spika Kaberia Arimba, ambaye alitoa habari hii ya tanzia, amesema MCA Gainchi alikuwa anaugua.

Mwanasiasa huyu alikuwa anapokea matibabu katika Hospitali ya Nairobi, ingawa haijabainishwa alichokuwa anaugua.

Gainchi ni MCA wa pili kuaga dunia wiki hii, baada ya Cyrus Omondi wa Kiambu.

Omondi alipatikana akiwa amefariki katika chumba chake cha hoteli nchini India, ambako alikuwa amesafiri na MCA wengine kwa ziara rasmi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *