[Video] Mhubiri Ng’ang’a Awashangaza Wengi, Adai Kumchumbia Mamake King Kaka

Mchungaji mwenye utata James Ng’ang’a amerejea kugonga vichwa vya habari, wakati huu, na tamko la kushangaza.

Mchungaji huyo, ambaye amekuwa akitawala vichwa vya habari mwaka huu, alishtua wengi baada ya kudai mamake mwimbaji wa kufokafoka ajulikanaye kama King Kaka, ni mchumba wake.

Mkuu wa kanisa la Neno Evangelism Centre, ambaye kwa sasa mkewe wa tatu, ambaye ni takriban nusu ya umri wake, alitoa usemi huo wa kushangaza wakati wa ibadi kanisani mwake.

Utani huo unakuja wakati rapa huyo amekuwa akitesa anga za usanii baada ya kuachilia wimbo wake mpya wa ‘kimapinduzi’ wa ‘Wajinga Nyinyi’ ambao unawashambulia wanasiasa kwa kuwa wafisadi.

King Kaka na mamake.

King Kaka amekuwa akimmiminia sifa mamake, Elizabeth Ombima, ambaye amekuwa akitokea kwenye kanda za video za nyimbo zake.

Babake, Julius Ombima, alifariki King Kaka akiwa na umwri wa miaka 16.

Akiongea kuhusu mamake, King Kaka hivi karibuni alielezea kwa nini mamake ni mfano mwema kwake.

” Niliulizwa juzi, ni nani mfano mwema wangu wa kuiga, nikasema mama yangu. Namaanisha, nani ‘hustler’ kama yeye, aliwalea wavulana watatu kwa kufanya biashara rejareja ya kuuza matunda….Mimi ni ‘hustler’ wa mwisho. Namaanisha Mandela alikuwa hodari kwa uongozi, Biko alikuwa mwenye hekima, Luther King alikuwa thabiti na uongozi wake, Obama na usemi wake, Maathai na maono yake, Ali kwa kujiamini kwake lakini hakuna anayemshinda mama yangu. Naye akamlea mfalme. Nakuvulia kofia Mama. Malkia Elizabeth. Shujaa kamili,” alisema King Kaka.

Ma come backs

Posted by Muthoni Mary Anne on Wednesday, 18 December 2019

Kufikia sasa, King Kaka wala mama yake hawajajibu taarifa hiyo ya kushtua ambayo bado imewaacha wengi wakijiuliza kwanini mchungaji alisema hivyo.

Tazama video hapa chini:

Pastor Ng'anga had some words for #KingKaka 😲😲

Posted by Nairobi Gossip Club on Thursday, 19 December 2019

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *