Rais Mstaafu Mzee Moi Amelazwa Hospitalini

President Uhuru Kenyatta during his visit to former President Daniel arap Moi and Baringo Senator Gideon Moi at his Kabarak home on Monday, April 22, 2019

Rais wa zamani Daniel arap Moi amelazwa katika Hospitali ya Nairobi kwa kile familia ilisema ni uchunguzi wa kawaida.

Taarifa kutoka kwa familia na hospitali vilieleza Star kwamba Moi alilazwa mnamo Ijumaa na anatarajiwa kukaa kwa siku kadhaa hospitalini kwa uchunguzi zaidi.

“Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi juu yuko hospitalini kwa uchunguzi wa kawaida na kuhudhuriwa na daktari wake Dr David Silverstein. Anatarajiwa Kulazwa siku kathaa ili kuwaruhusu madaktari muda wa kutosha wa kukagua Mzee, “alisema msemaji wa ndani

Katibu mkuu wa Kanu Nick Salat alithibitisha kwamba Moi alilazwa.”Ndio yuko Hospitalini ila tu ni kwa uchunguzi wa kawaida,” Salat, ambaye aliteuliwa mnamo Aprili, kama mwenyekiti wa Shirika la Posta, aliiambia Star kwa simu.

Image result for mzee moi recent images

 

Lakini wakati Star ilipowasiliana na katibu wa vyombo vya habari vya Moi, Lee Njiru, alisema hakujua Rais wa zamani alikuwa mgonjwa na hospitalini.”Nipo Nakuru na sijui ripoti kama hizi. Nitauliza na nitawajulisha mara nitapata ripoti hiyo,” Njiru aliwambia Star kwa simu.

Kulazwa kwa Moi kunakuja siku baada ya Wakenya kusherehekea kurudi kwa Siku ya Moi, likizo ya umma aliyoianzisha.

Siku ya Moi iliondolewa katika orodha ya likizo za kitaifa kufuatia kutangazwa kwa Katiba mnamo Agosti 2010.

Lakini Mahakama Kuu ilirudisha siku hiyo kuwa likizo kwa sababu ya kuondolewa kwake ilikuwa kukiuka Sheria ya Likizo ya Umma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *