Wakenya Wamkejeli Ruto baada ya Kuahidi Kujenga Shule kwa Muda wa Miezi Mitatu

Masaa kadhaa tu baada ya kuahidi kwamba serikali itaunda shule mpya ya msingi ya umma katika eneo la Ngando, Dagoretti Kusini, chini miezi mitatu, Naibu wa Rais Wiliam Ruto amekejeliwa na sehemu ya watumizi wa mtandao.

Wakenya hao katika mtandao walionekana kutoridhika na ahadi za makamu wa rais hukuwa wakimshutuma kwa kuchuma umaarifu palipo na mkasa.

Ruto, kupitia ukurasa wake ya Twitter, alithibitisha kuwa Idara ya Kazi ya Umma na Elimu ya Serikali, kwa kushirikiana na bodi ya Shule ya Lenana walikuwa kwenye harakati za kujenga shule ya msingi ya umma katika eneo hilo.

Alisisitiza kuwa shule hiyo inatarajiwa kuwa tayari mwanzoni mwa Januari kwa lengo la kuhudumia watoto wa Ngando, ambapo janga la Precious Talent School lilitokea Jumatatu.

“Idara za Jimbo la Kazi za Umma, Elimu na NYS zitashirikiana na Bodi ya shule ya Lenana kujenga shule ya msingi ya umma ili kuwasaidia watoto wa eneo la Ngando ambapo janga la shule hiyo lilitokea. Mchakato huo ulianza asubuhi ya leo kwa dhati ” alihakikisha Naibu wa Rais.

Uhakikisho wa Ruto  unafuatia kuporomoka kwa darasa la Precious Talent School, ambalo  wanafunzi saba walifariki na zaidi ya 64 kuuguza mejaraha.

Tukio hilo lilitokana na ujenzi duni wa majengo ya darasa.

Licha ya kutembelea shule iliyoathiriwa Jumatatu jioni na kuahidi ujenzi wa shule hiyo mpya, wakenya walimkejeli na kumkubusha ahadi ambzo alikuwa bado hajatimiza.

Pamoja na hayo, Ruto alihakikishia kwamba Wizara ya Elimu ilikuwa inafanya ukaguzi ili kuhakikisha usalama wa majengo yote ya shule nchini kote ili kuzuia matukio ambayo yanaweka maisha ya wanafunzi hatarini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *