Mtambue Katibu Mkuu ‘Anayeogopwa’ zaidi Serikalini… Maelezo kwa Kina

Kwa mwanaume ambaye ni nadra kushiriki katika mahojiano na vyombo vya habari, Dk Karanja Kibicho hivi karibuni ametawala vichwa vya habari baada ya wanasiasa wengi kutoa shutma mbali mbali dhidi yake.

Naibu wa Rais William Ruto, mtu wa pili aliye na nguvu zaidi nchini, ameripotiwa kuhusika katika mizozo miwili na Katibu huyo mkuu wa wizara ya Mambo ya Ndani.

Katika kisa cha kwanza, kinachosemekana kutokea katika uwanja wa ndege wa JKIA, Naibu wa Rais alidai kwamba Kibicho alikuwa ameamuru kutolewa kwa  vyombo zya usalama kutoka mikutano ya kampeni za Ruto kote nchini.

Katika kisa cha pili, inasemekana kuwa Ruto alitoa malalamishi dhidi ya Kibicho na viongozi wengine kadhaa kutoka eneo la Mlima Kenya kwa tuhuma za kutishia maisha yake.

Katika visa vingine vingi, wanasiasa wanaohusiana na Ruto wameendelea kutoa madai dhidi ya Kibicho. Hivi majuzi, mbunge wa Kandara, Alice Wahome alidai kuwa maisha yake na ya Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro yako hatarini baada ya kumshutumu Kibicho kuwa alikuwa akiwapangia njama ya kuwamaliza.

Labda kwa sababu ya mashtaka dhidi yake, Kibicho mara nyingi hajishughlishi kujibu kupitia vyombo vya habari ambapo mengi ya tuhuma hizi hutolewa – wahandisi wanasemekana kuwa waja wenye maneno machache.

Kabla ya 2010, Katibu mkuu huyo alikuwa hajulikani nje ya ukumbi wa madarasa ya taaluma ya masomo ya uhandisi.

Nafasi yake katika utafiti ilionekana wazi katika ubunifu wa matumizi ya maganda ya mchele na kahawa kuunda mikoko ya makaa yasiyoharibu mazingira. Kibicho pia aliisimamia Idara ya Uhandisi wa Mitambo katika Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT).

Mnamo mwaka wa 2010, Rais Mwai Kibaki – kutokana na mapendeleo yake kwa wasomi – alimfanya Kibicho kuwa katibu mkuu wa Viwanda vya Ustadi.

Miaka mitatu baadaye, baada ya kuchaguliwa kwa Rais Uhuru Kenyatta mnamo 2013, mhandisi huyo kutoka Kirinyaga aliondolewa kutoka ufanisi wake, wa maendeleo ya viwanda, na kutupwa katika ulimwengu wa diplomasia kama katibu mkuu wa Masuala ya Mambo ya nje.

“Ninaelewa kuwa mataifa hayashirikiani kwa upendo wa kimapenzi,mbali  hufanya hivyo ili kufikia masilahi ya pamoja,” aliliambia Bunge wakati wa kuhojiwa.

Hotuba zake mara nyingi hufanywa na tabasamu, licha ya uzito wa maswala anayozungumzia .Katika tukio moja, muda mfupi baada ya kuhamia wizara ya Mambo ya ndani, Kibicho alikuwa kwenye shughuli za kumaliza uuzaji wa pombe haramu katika mkoa wa Mt Kenya. Wakati mmoja, alihutubia mkutano wa hadharani ambapo machifu  ambao maeneo yao yalikuwa wameathiriwa na uuzaji wa pombe haramu walihudhuria.

“Kuna wachifu wawili hapa. Mmoja ni Weston Ngiria na mwingine ni Dickson Kimama, tafadhali rudisha sare zangu, “Kibicho aliwaamrisha huku machifu hao wawili akitii amri na kuvua kofia na shati zao rasmi.

Ilikuwa onyesho la tabia ya madhubuti isiyo banduka wala kutishika.

Mwaka jana, Dennis Wachira, mchuuzi katika mji wa Nairobi, alivuma katika mitandao ya kijamii baada ya kutoa madai kuwa Rais Kenyatta alikuwa na deni lake la Shilingi 40, baada ya kumuuzia pipi akiwa kwenye msafara wa kampeni.

Kibicho alimpa mualiko mchuuzi huyo aenda afisini mwake Harambee House. Hata hivyo,  Wachira hakuyaamini macho yake baada ya Kibicho kumpa noti ya Sh50 na kudai salio mbele ya wanahabari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *