IEBC yatupilia mbali Ugombea wa Mariga

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imetupilia mbali ugombea wa MacDonald Mariga.  Hii inatokana na maelezo yanayokosekana kutoka kwa sajili wa wapigakura.

Jaribio la Seneta wa zamani wa Kakamega Boni Khalwale na mbunge Nixon Korir kujadiliana na IEBC juu ya suala hilo halikuzaa matunda yoyote baada ya afisa wa IEBC Beatrice kusimama kidete juu ya suala hilo.

Hapo awali, Mariga alikuwa ametuzwa cheti cha uteuzi na Jubilee kabla ya kuendea idhini kwa IEBC .Hata hivyo, alikuwa ametayari ameanza kufanya

Tukio hilo la hivi karibuni litakuwa pigo kubwa kwa Jubilee ambao na matumaini makubwa kwa mchezaji huyo wa zamani wa Soka.Sio mara ya kwanza wakati ugombea wa Mariga anakabiliwa na shida.

Imran Okoth

Katika rufaa ambayo tayari imetupiliwa mbali, mmoja wa wagombea wa Jubilee katika kiti hicho, Peter Peter Kinyajui, alidai kuwa Mariga hakuwa amesajiliwa kama mpiga kura.

“Kuongeza utata zaidi, mtu aliyechaguliwa sio mkazi au mpiga kura wa eneo bunge la Kibra na kuna mashaka makubwa iwapo ameshawahi kupiga kura,” alisema.

“Ugombea wake hautaweza kuuza sera za watu wa Kibra kutokana na sifa ya mbunge tuliyekuwa naye hapo awali.”

Wakati huo huo, IEBC imeidhinsha zaidi ya wagombea 10 kutoka vyama tofauti vya kisiasa kushiriki katika uchaguzi utakaofanyika mnamo Novemba 7.

Kati ya wale walioidhinshwa ni pamoja na Bernard Okoth wa ODM na mgombea wa Ford Kenya Khamisi Butich

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *