CMB Prezzo Kuwania Ubunge wa Kibra

Image result for cmb prezzo

Mwanamuziki wa Kenya Jackson Makini maarufu kama Prezzo ametangaza azimio lake la kuwania kiti cha ubunge wa Kibra.

Prezzo, ambaye amekichagua chama cha Wiper kama Chombo cha kuwania ubunge , alifunuliwa na Makamu wa Rais wa zamani Kalonzo Musyoka mnamo Jumanne alasiri.

Kalonzo ameonyesha imani kuwa mwanamuziki huyo atapata ushindi mnamo Novemba 7 . Hata hivyo amesisitiza kuwa hatua hiyo haiashirii kuvunjwa kwa muungano wa NASA.

Prezzo, ambaye aliambatana na kikundi cha vijana kutoka Kibra, aliahidi kutekeleza miradi ya maendeleo iwapo atachaguliwa.

Hii inakuja masaa kadhaa baada ya ODM na Jubilee kuwasilisha vyeti kwa Imran Okoth na Macdonald Mariga mtawalia.

Kiongozi wa chama Raila Odinga alikuwepo wakati wa hafla ya uwasilishaji wa cheti na kujumuika na wagombea wengine kumi ambao walikuwa wameshiriki katika kura ya mchujo ya chama cha ODM.

Wagombea waliochujwa walielezea kwamba kaka wa marehemu Ken Okoth alikuwa na baraka yao kamilifu, baada ya kukubali kushindwa wakati wa uchaguzi wa chama uliofanyika Jumamosi.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa ODM Junet Mohammed alisema kwamba wana uhakika watashinda uchaguzi kwa sababu ODM ndio chama pekee ambacho kilifanya uchaguzi huru na wenye haki

“Kile chama ambacho kimefanya nominations nchini katika uchaguzi huu wa Kibra ni ODM; wale wengine hawakufanya nominations…walifanya selection! Nawaambia Jubilee, ANC, Tangatanga na hao wengine wajitayarishe kwani Kibra ni ODM” Junet alisema.

Prezzo, Imran, Mariga na Owalo watamenyania kiti hicho  mnamo Novemba 7.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *