Askofu wa Katoliki aweka sheria Kali dhidi ya Wanasiasa Kanisani

Team Kieleweke and Tangatanga members clash at a church in Murang'a on Sunday, September 8, 2019.

Askofu wa Murang’a amewaambia wanasiasa waliohusika katika mzozo katika mkutano wa kanisa Jumapili kuomba msamaha hadharani.

Askofu James Wainaina katika taarifa kwa waandishi wa habari Jumatatu alisema wakati umefika wa wanasiasa kutengwa kwa shughuli za kanisa. Alisema uamuzi huo atatekelezwa katika majimbo yote , Jimbo la Muranga likiwa mojawapo.

Wainaina alisema kufuatia tukio hilo lililovuruga ibada ya kanisa hilo , ni dhahiri kwamba wanasiasa hawana maadili ya dini za kikristo. Alisema wanasiasa kwa miaka mingi wamechukulia mikusanyiko ya Kikristo kwa hadhi ya chini. Pia alisema kuwa wanasiasi wameyageuza makanisa kuwa majukwaa ya kujishughulisha na kujipendekeza kisiasa.

“Ninahisi tukio hili lilikuwa thibitisho dhabiti kuwa wanasiasa wanafaa kuwekewa vikwazo wakati wa kuhutubia waumini kanisani,” alisema.

Alisema tukio hilo linathibitisha zaidi umuhimu wa mikusanyiko ya wakristo kubaki mikononi mwa Askofu au kuhani.

“Hii imetupa tahadhari kuwa tukio ambalo linaweza kuonekana bila hatia  mwanzoni linaweza kuwa mbaya na la aibu ikiwa watu wasiofaa watasimamia mikusanyiko kama haya,” alisema.

Wainaina aliendelea kusisitiza kuwa kanisa ni chumba cha sala na lazima kiheshimiwe.

Uamuzi huu, unafuatia kisanga cha Jumapili kati ya mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro, mwanachama wa Tangatanga, kugongana na timu ya Kieleweke katika kanisa moja la kikatoliki katika eneo hilo. Alisema tukio hilo ni la kusikitisha na la aibu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *