Joe Mwangi hatimaye Amekamatwa

Wendy Waeni's ex-manager Joe Mwangi

Aliyekuwa meneja wa Mwanasarakasi Wendy Waeni, Joe Mwangi amekamatwa.

Kulingana na Ukurasa wa DCI wa Twitter Jumatatu, Mwangi atashtakiwa mara tu mchakato ufaao wa polisi utakapokamilika. DCI iliwashukuru Wakenya kwa kusiadia kwa kutoa  habari juu ya alipokuwa Mwangi.

Mwangi anatuhumiwa kwa kumlaghai Waeni.

Wachunguzi kutoka Kitengo cha Ulinzi wa Mtoto walianza kuchunguza suala hilo mwezi uliopita baada ya Waeni kutokea kwenye Citizen TV na kusema yeye na mama yake walikuwa wakiishi masikini licha ya kufanya sarakasi kote ulimwenguni.

Waeni alisema, “Nimefanya cheza kote ulimwenguni lakini sijafaidi na hata senti kutoka kwake na hiyo ni kwa sababu ya meneja wangu wa zamani.” Msichana huyo alisema alikuwa akiishi katika chumba kimoja pamoja mama yake katika makao ya Huruma, Nairobi.

Wendy ni Mwanasarakasi na pia Balozi wa Unicef na amewachezea Marais pamoja na Uhuru Kenyatta na Paul Kagame wa Rwanda.

Wendy alisema mama yake anauza pipi na sigara usiku kucha ili kupata pesa za kulipa kodi. Walakini, wakati wa mahojiano na Radio Jambo, mama wa Waeni alikiri Mwangi alimpatia “pesa kidogo”.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *