Rais pekee ndiye ana Uwezo wa Kutoa Amri ya Kuondoa Wakaazi Mau: Murkomen

A file photo of Elgeyo Marakwet Senator Kipchumba Murkomen. /STEPHEN RUTTO

Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen amesema hakuna mtu mwengine isipokuwa Rais Uhuru Kenyatta, anaweza kutoa amri ya kufukuzwa kwa Wakaazi kutoka ardhi ya Mau.

Kiongozi Wa Wengi katika Seneti alisema kupitia ukurasa wake wa Twiiter Jumatatu kuwa hata  Waziri wa Mazingira Keriako Tobiko hana uwezo wa kutoa amri hiyo.

“Hakutakuwa kuondoka kutoka kwa Masai Mau Trust Land hadi Rais Uhuru Kenyatta atakapozungumza,” Murkomen alisema.

Aliongeza kuwa Tobiko hana mamlaka ya kuwafukuza watu kutoka eneo hilo. Murkomen aliwasihi watu wa Mau kuendelea na maisha yao ya kila siku na kuwapeleka watoto wao shuleni kuendelea na Muhula wa tatu.

Kauli yake amechipika huku awamu ya pili ya kuwaondoa watu katika eneo hilo ikitarajiwa kuanza, zaidi ya watu 60, 000 wanahofiwa kuadhirika. Sehemu ya viongozi kutoka Bonde la Ufa wameiomba serikali kushughulikia suala la Mau kwa njia ya ubinadamu.

Kupitia taarifa Jumamosi, walisema awamu ya pili ya kufukuzwa inaweza kuwaadhiri zaidi ya wanafunzi 10,000. Tobiko alikuwa ametangaza kuwa hifadhi ya Mau imeanza na haitasitishwa, akitoa ilani wa siku 60 kwa wakaazi wasio halali kupisha njia.

Mnamo Julai 25, Tobiko aliapa kuendelea na uhamishaji, akisema hakuna kiwango chochote cha vitisho kinachoweza kuizuia.

Hii hapa kauli ya Murkomen

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *