Fahamu kaka wa Matiang’i anayetikisa KNUT

Image result for john matiangi

Wakenya wengi wanafahamiana na waziri wa Mambo ya Ndani Fred Matiang’i kwa sababu ana cheo kubwa kwenye serikali ya Uhuru Kenyatta.

Walakini, ni wachache tu wanajua kuwa Matiang’i ana kaka yake ambaye pia anashikilia moja ya ofisi za juu nchini Kenya.

John Matiang’i ni hazina wa kitaifa katika Jumuiya ya Walimu ya Kitaifa (KNUT) na alikuwa mmoja wa watu muhimu ambao walishawishi kuondolewa kwa mkurugenzi Wilson Sossion kwenye umoja huo.

Hata hivyo, John Matiang’i ni mtuliu kinyume na fred Matiang’i lakini pia amegonga vichwa vya habari mara kadhaa.

Image result for john matiangi

Mnamo Mei 2018, alikataa kazi ya kuvutia ya serikali ; kuwa kamishna wa Tume ya Mishahara na Malipo (SRC).

Kulingana na ripoti, alikataa kukubali uteuzi kwani msimamo huo ungemhitaji afanye kazi muda wote.

Mnamo mwaka wa 2017, alizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya familia yao kwa  madai ya kwamba nyumba ya Fred Matiang’i ilikuwa imechomeka baada ya picha kadhaa kusambaa mtandaoni.

Mnamo 2004 hadi 2008, John alipata digrii yake ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Shahada ya Elimu katika Kiswahili na Jiografia.

Kisha alijiunga na Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki, Baraton, kwa shahada ya juu katika Utawala wa elimu mnamo 2010-2013.

Alimaliza masomo yake na PhD katika Chuo Kikuu cha Nairobi ambapo alikua Daktari wa Falsafa katika Utawala wa elimu.

Image result for john matiangi

Ndugu ya Matiang’i alijiunga na Tume ya Huduma ya Ualimu kwa miaka 14, kuanzia 1990-2000. Alikua Mwalimu Msaidizi kwa miaka sita na Mwalimu Mkuu wa Msaidizi kwa miaka nne. Akawa Mwalimu Mkuu kati ya 2000 na 2004.

Alijiunga na tume ya KNUT mnamo 2008, ambapo alikua Katibu mtendaji wa Tawi kwa miaka 6.

Mnamo 2014, alikua Mweka Hazina wa Kitaifa wa umoja huo, nafasi ambayo anashikilia sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *